Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bara la Afrika liko njiani ya kutokomeza polio

Bara la Afrika liko njiani ya kutokomeza polio

Ni mwaka mmoja tangu kisa cha mwisho cha ugonjwa wa kupooza au polio kilipobainiwa barani Afrika, hii ikiwa ni hatua kubwa katika kutokomeza ugonjwa huo, limesema Shirika la Afya duniani WHO.Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa Joshua)

WHO imeeleza kwamba kisa cha mwisho cha polio kilitokea nchini Somalia tarehe 11, Agosti, mwaka 2014.

Aidha WHO imesema kuwa hakukuwa na kisa cha ugonjwa wa kupooza nchini Nigeria tangu Juni mwaka 2014, nchi hii ikiwa ni ya kwanza barani Afrika kwa kuathirika na ugonjwa huo.

Shirika hilo limeongeza kuwa iwapo kisa kingine hakitagundulika katika kipindi cha miaka miwili ijayo, basi bara la Afrika litathibitishwa kwamba limetokomeza ugonjwa huo.

Bado nchi mbili duniani zinakumbwa na maambukizi ya ugonjwa wa kupooza zikiwa ni Afghanistan na Pakistan.