Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwajibikaji na mazungumzo jumuishi ndio muarobaini wa ustawi Burundi- Ban

Uwajibikaji na mazungumzo jumuishi ndio muarobaini wa ustawi Burundi- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesisitiza kuwa uwajibikaji na kurejelea mazungumzo ya kisiasa ya kweli na jumuishi ndiyo njia bora ya kukabiliana na majaribio ya kusambaratisha ustawi nchini Burundi. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Katibu Mkuu amelaani vikali jaribio la mauaji dhidi ya Pierre Claver Mbonimpa, mtetezi maarufu wa haki za Binadamu nchini Burundi, ambaye alifyatuliwa risasi na watu wasojulikana hapo jana.

Bwana Ban amemtakia nafuu haraka, na kutoa wito uchunguzi wa wazi ufanywe hima ili kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria.

Ban amesema kitendo hicho kilichotokea siku moja baada ya kuuawa kwa Jenerali Adolphe Nshimirimana, ni sehemu ya mwenendo unaoenea wa ukatili wa kisiasa nchini Burundi, ambao unapaswa kukomeshwa kabla ukithiri.