Skip to main content

Vikwazo vya usafiri vyazuia misaada Sudan Kusini: OCHA

Vikwazo vya usafiri vyazuia misaada Sudan Kusini: OCHA

Marufuku iliyowekwa na mamlaka  dhidi ya mashua kutoka Malakal mtoni Nile, pamoja na uhaba wa waongozaji wa ndege kwa ajili ya kutumia eneo la kuruka na kutua ndege vinakwamisha operesheni ya misaada jimboni Upper Nile imesema ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA.

Kwa mujibu wa OCHA hali nchini Sudani Kusini ni mbaya hususan jimboni Malakal ambapo watu takribani 65,000 wametahiriwa na vikwazo hivyo vya usafiri huku mashirika ya kibinadamu yakiripoti upungufu wa madawa, mafuta na kemikali za maji.

Ofisi hiyo imesema majadiliano yanaendelea ili kuhakikisha misaada inafika Upper Nile ili kuepuka kuzorota zaidi kwa hali .

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu misaada ya kibinadamu na mkuu wa OCHA Stephen O'Brien, ametaka kufikishwa kwa misaada hiyo  hima akisema kuwa alivyokuwa nchini Sudan Kusini alimtaka Rais wa nchi hiyo  Salva Kiir kusaidia katika kuondoa vikwazo hivyo.