Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yalaani shambulio dhidi ya gari la msaada wa chakula CAR

OCHA yalaani shambulio dhidi ya gari la msaada wa chakula CAR

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu ya misaada ya kibinadamu OCHA nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, imelaani vikali shambulio dhidi ya msafara wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP mnamo Julai 18 mwaka huu.Taarifa kamili na Priscilla Leciomte(TAARIFA YA PRSCILLA)

Ikimnukuu mkuu wa OCHA  nchini CAR Marc Vandenberghe, taarifa ya shirika hilo imesema msafara huo uliosindikizwa na walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA ili kuwafikishia misaada waathirika Kaskazini mashariki mwa CAR umeshambuliwa na kusababisha gari kupoteza mwelekeo na kurudi nyuma.

Watu wengine katika msafara huo wamejeruhiwa.

Amadou Toure, msemaji wa MINUSCA anafafanua zaidi.

(SAUTI AMADOU)

‘‘Misafara inasindikizwa na kikosi cha MINUSCA kwa ajili ya usalama, lakini mara kwa mara misafara ni mirefu mno na hatuwezi kuweka wanajeshi kila sehemu. Kwa hiyo ni watu waliojihami walioshambulia msafara huo, wakampigia risasi tatu dereva ambaye bahati mbaya amefariki dunia baada ya kujeruhiwa.  ‘’

 OCHA imetuma salamu za rambirambi kwa waathiriwa wa shambulio hilo na kuwatakia uponyaji wa haraka majeruhi.