Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa kujikwamua na Ebola uende sambamba na ule kukabili ugonjwa: Dkt. Nabarro

Msaada wa kujikwamua na Ebola uende sambamba na ule kukabili ugonjwa: Dkt. Nabarro

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola Dokta David Nabarro amesema jamii ya kimataifa haiwezi kusubiri hadi Ebola itokomezwe kabisa huko Afrika Magharibi ndipo ianze kutoa misaada.

Amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani, siku ya Alhamisi, kuhusu mkutanowa kimataifa wa kujadili jinsi ya kukwamua nchi hizo utakaofanyika Ijumaa, mkutano ambao umeitishwa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon.

Dkt. Nabarro amesema hadi sasa harakati kutokomeza Ebola zinaendelea vyema kwani hata idadi ya visa vipya si ya kutisha na uwezo wa kufuatilia pale ambapo vinaibuka ni mkubwa akitolea mfano kisa kimoja kilichoripotiwa Liberia.

Amesema usaidizi hatua dhidi ya Ebola na zile za kujikwamua zinaenda pamoja kwa kuwa..

(Sauti ya Nabarro)

Lazima huduma za afya zirejee ili kuweza kurejesha imani ya watu wanaorejea na iwapo maisha na hali ya kujipatia kipato vinatakiwa kurejea katika hali ya kawaida.”

Kwa hiyo katika mkutano huo..

(Sauti ya Nabarro)

“Unatarajiwa kupata ahadi za kifedha kama mchango wa kutekeleza mikakati ya kitaifa na kikanda ambayo itajikita katika kipindi cha miaka miwili.

Katika kikao hicho Katibu Mkuu Ban Ki-moon sambamba na marais wa Liberia, Sierra Leone na Guinea ambao nchi zao zimeathiriwa zaidi na mlipuko wa Ebola watasikiliza hatua za kujikwamua hadi sasa na mipango ya baadaye