Ban akutana na kuzungumza na waziri wa mambo ya kigeni wa Norway

6 Julai 2015

Akiwa Norway Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Norway Børge Brende, na kumshukuru kwa mchango wa nchi yake kueleka katika mkutano wa maendelo ya elimu mjini Oslo.

Katibu Mkuu na waziri huyo wamekubaliana kuhusu hitaji la dharura kwa nchi wanachama kuvuka vikwazo vya mwisho katika majadiliano kabla ya uwezeshaji wa kifedha unaofunguliwa juma lijalo mjini Addis Ababa Ethiopia.

Kadhalika wamebadilishana mawazo kuhusu mkutano wa maendeleo endelevu mjini New York na kusisitiza kuwa suala la mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi mjini Paris Ufaransa ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya dunia.

Bwana Bana amemefahamisha  Bwana Brende kuhusu juhudi za Umoja wa Mataifa za kusaka suluhu ya kudumu kwa mgogoro wa Syria na kukomesha mgogoro nchini Yemen ikiwamo kwa kusimamisha mapigano.  Viongozi hao pia walijadili hali ya sasa katika mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter