Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yasisitiza kutokomeza Ukimwi ifikapo 2030

UNAIDS yasisitiza kutokomeza Ukimwi ifikapo 2030

Mkutano wa 36 wa  bodi ya uratibu ya shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha  na mapambano dhidi ya Ukimwi UNAIDS umemalizika mjini Geneva Uswis kwa kuweka mkazo wa kuimarisha uwekezaji na matokeo katika kipindi cha miaka mitano ijayo ikilenga kumaliza janga hilo ifikapo mwaka 2030.

Katika kikao chake bodi hiyo pia imesisitiza umuhimu wa kuimarisha juhudi za kushughulikia ugonjwa wa Ukimwi katika ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 na kukuza maendeleo ya mkakati wa UNAIDS wa mwaka 2016 hadi 2021.

Wajumbe wa bodi wametambua pia umuhimu wa kuwa na hatua madhubuti katika kushughulikia usambaaji wa HIV kupitia sindano na kwamba kuelekea mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa wa mwaka 2016 kuhusu tatizo la madawa bodi imepitisha maamuzi ya kijasiri na kutaka nchi kutekeleza sera yakinifu za madawa zinazoheshimu haki za binadamu na kukuza afya ya jamii .

Mkurugenzi Mkuuu wa UNAIDS Michel Sidibe amesisistiza fursa iliyoko katika kautokomeza ukimiwi akisema kuwa ikiwa malengo ya kasi yatafikiwa ifikapao mwaka 2020 janga hilo litaisha ifikapo mwaka 2030.