Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalaani shambulio dhidi ya kambi ya AMISOM Somalia.

Baraza la usalama lalaani shambulio dhidi ya kambi ya AMISOM Somalia.

Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali shambulio la kigaidi katika Kambi ya Leego,  ya ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM, lililotekelezwa na kundi la kigaidi la Al-Shabaab mnamo Julai 26 na kusababisha vifo na majeruhi miongoni mwa walinda amani kutoka Burundi.

Wajumbe wa baraza la usalama katika taarifa yao wameelezea huzuni na  rambirambi zao kwa familia za waathiriwa, watu na serikali ya Burundi, AMISOM na serikali ya Somalia huku pia wakilaumu Al-Shabaab kwa shambulio katika kambi hiyo ya AMISOM inayofanya kazi na serikali ya shirikisho la Somalia, jeshi la taifa la nchi hiyo ili kuwalinda watu wa Somalia na kusadia katiak ujenzi na utulivu wa taifa hilo.

Wajumbe wa baraza wamesisitiza kuwa ugaidi kwa namna yoyote ile husababaisha moja ya tishio kubwa kwa amani ya kimataifa na usalama na kuwa vitendo vya ugaidi ni uhalifu usiokubalika bila kujali nia yake, mahali, muda na nani katekeleza.