Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashauriano kuhusu Yemen huko Geneva, ni mwanzo mzuri lakini safari ndefu:

Mashauriano kuhusu Yemen huko Geneva, ni mwanzo mzuri lakini safari ndefu:

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed amesema amelieleza Baraza la usalama kuwa mashauriano kuhusu Yemen yaliyohitimishwa hivi karibuni huko Geneva ni mwanzo mzuri wa kuanzisha tena mchakato wa kisiasa.

Amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha faragha cha Baraza hilo la usalama akisema kitendo cha pande husika kwenye mzozo huo kushiriki mashauriano ya Geneva ni hatua kubwa lakini kilichomgusa zaidi ni kwamba..

(Sauti ya Ould)

“Ninasikitishwa sana na mgawanyiko mkubwa baina ya pande husika na kutokuwepo kwa hali ya kulegeza misimamo jambo ambalo lilisababisha kushindwa kufikia makubaliano ambayo yalikuwa karibuni kupatikana.”

Hivyo amekumbusha kuwa..

(Sauti ya Ould)

Kwa mara nyingine tena napenda kuwakumbusha kuwa mashauriano ya awali ya Geneva yalikuwa ni mwanzo wa kuzindua mwelekeo mrefu na mgumu wa kurejesha Yemen katika mchakato wa siasa. Natambua kuwa kurejesha mchakato huo haitakuwa rahisi.”

Yemen imekuwa katika mzozo tangu kikundi cha Houthi kitwae mji mkuu Sana’a mwezi Septemba mwaka jana na kusababisha Rais na viongozi wengine wa serikali kusaka hifadhi huko Riyadh.

Mapigano yamekuwa yakiendelea nchini Yemen na kusababisha maelfu ya raia kusaka hifadhi nchi jirani ikiwemo Djibouti na wengine Somalia.