Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO na wizara ya afya ya Korea vyafuatilia mlipuko wa Corona

WHO na wizara ya afya ya Korea vyafuatilia mlipuko wa Corona

Shirika la Afya duniani WHO pamoja na wizara ya Afya ya Jamhuri ya Korea wametangaza leo mapendekezo yao ya awali kuhusu mlipuko wa homa ya kirusi cha Corona nchini humo, baada ya kuanza ujumbe wao wa pamoja wa utafiti hapo jana.

Kwa mujibu wa WHO, tayari visa 108 vya homa hiyo vimethibitishwa nchini Korea Kusini , na hadi sasa watu Tisa wamefariki dunia.

Mapendekezo yaliyotolewa ni pamoja na kuimarisha harakati za kuzuia maambukizi, kupima wagonjwa kwenye vituo vyote vya afya nchini humo na kuzuia usafiri wa watu waliokuwa karibu na wagonjwa.

Hata hivyo ujumbe huu wa pamoja umependekeza kufungua upya shule, kwa sababu utafiti unaonyesha kwamba si sehemu hatari ya kusambaza ugonjwa huo.

Ujumbe huo wa pamoja unatarajia kumaliza utafiti wake nchini humo tarehe 13 mwezi huu.