Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taasisi ya Sasakawa na WHO zapigia chepuo Ukoma utokomezwe duniani

Taasisi ya Sasakawa na WHO zapigia chepuo Ukoma utokomezwe duniani

Wakati kikao cha nane kuhusu mkataba wa haki za watu wenye ulemavu kinaendelea mjini New York, swala la ukoma linazungumzwa leo kwenye mjadala maalum unaoandaliwa na idara ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa pamoja na serikali ya Japan na Ethiopia.

Kwa mujibu wa Shirika lisilo la kiserikali ya Japan, The Nippon Foundation, ukoma ni ugonjwa wa zamani lakini mpaka sasa wagonjwa wake wanaendelea kutengwa na jamii na kunyanyapaliwa, wakati huu ambapo tiba dhidi yake inapatikana, na tayari watu milioni 16 duniani wameshatibiwa tangu miaka ya 80.

Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa, Yohei Sasakawa, mwenyekiti wa taasisi hiyo ya Nippon, na Balozi mwema wa Shirika la Afya Duniani WHO kuhusu ukoma, amesema

(Sauti ya Sasakawa)

“ Ukiangalia ukoma, ni ugonjwa wa aina yake. Ukiulinganisha na pikipiki, kutibu wagonjwa ni gurudumu la mbele, na gurudumu la nyuma ni kupambana na unyanyapa na ubaguzi Kwa hiyo matibabu pamoja na kupambana na unyanyapaa vinapaswa kwenda sambamba ili kutokomeza ukoma.