Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujifungua kwa upasuaji sasa ni mtindo, lakini kuna hatari: WHO

Kujifungua kwa upasuaji sasa ni mtindo, lakini kuna hatari: WHO

Shirika la afya duniani, WHO limeonya kuhusu utamaduni ulioshamiri sasa kwa baadhi ya madaktari, wanawake kupenda huduma ya upasuaji wakati wa kujifungua likisema kuwa licha ya kwamba huduma hiyo ni muhimu kuokoa maisha ya mama na mtoto ni lazima izingatie vigezo vyake.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi, Dokta Marleen Temmerman wa WHO amesema ni dhahiri kuwa uzazi kwa njia ya upasuaji unaweza kuokoa maisha lakini mara nyingi hufanyika bila ulazima na madaktari na wazazi wanaona ni rahisi kuliko kujifungua kawaida.

Mathalani amesema inapaswa itumike iwapo kujifungua kwa njia ya kawaida kunahatarisha maisha  ya mama pengine amepata uchungu wa kupitiliza au mtoto hayupo katika nafasi nzuri ya kutoka kawaida hivyo akasema…

(Sauti ya Dkt. Tammerman)

Ni kwamba hatupaswi kufanya upasuaji kwa kila mama anapojifungua. Jambo muhimu ni kwamba tunaamua njia ya kujifungua kawaida na tunaamua tu upasuaji iwapo kuna  muhimu kwa ajili ya afya ya mama na mtoto.”

Miongoni mwa madhara yatokanano ya kujifungua kwa upasuaji ni kutoka damu kupita kiasi, ulemavu na hata kifo iwapo huduma hiyo itafanyika katika maeneo yasiyo na vifaa vya kutosha na salama.