Kikao cha Kamisheni juu ya hali ya wanawake chaanza New York

Kikao cha Kamisheni juu ya hali ya wanawake chaanza New York

Kikao cha Kamisheni juu ya hali ya wanawake kimeanza leo mjini New York.

Wawakilishi wa serikali pamoja na makundi ya kiharakati zaidi ya 1,500 wanaweka zingatia lao kwenye majadiliano kuhusu nafasi ya mwanamke na mtoto wa kike kushiriki kwenye elimu, mafunzo na maeneo ya sayansi.

Ama kitengo cha Umoja wa Mataifa ambacho kimeanzishwa kwa ajili ya kushughulia masuala ya wanawake kitazinduliwa rasmi hapo alhamisi na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo hicho Michelle Bachelet anatazamiwa kutoa hutuba maalumu.

 

Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro naye atahutubia mkutano huo ambao unamalizika rasmi March 4.