Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali yazidi kuzorota Ukraine: Simonovic

Hali yazidi kuzorota Ukraine: Simonovic

Ripoti za hivi karibuni za ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu zinaonyesha kuwa chuki na madhila vinazidi kuongezeka miongoni mwa jamii zilizoathiriwa na mzozo nchini Ukraine.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kando mwa mkutano wa 28 wa baraza la haki za binadamu  msaidizi wa  Katibu Mkuu kuhusu haki za biandamu Ivan Simonovic amesema kuendelea kwa mgogoro huo husuan Mariupol kutasababaisha hali mbaya zaidi.

(Sauti ya Simonovic)

“Kama kuna kampeni ya kijeshi Mariupol, kutaleta majibu makali kutoka jumuiya ya kimataifa.”

Amesema mashambulizi ya silaha nzito mwezi Januari mjini humo yamesababisha vifo vya watu 31.

Kwa mujibu wa takwimu za kamishina wa haki za binadamu  Umoja wa Umoja wa Mataifa  tzaidi ya watu 5,000 wameuwawa tangu mwezi Aprilhadi February 15 huku zaidi ya milioni moja wakiwa hawana makazi kutokana na machafuko nchini humo