Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa IAEA awasilisha ripoti kwenye bodi ya magavana

Mkuu wa IAEA awasilisha ripoti kwenye bodi ya magavana

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomic (IAEA) bwana Yukiya Amano leo amewasilisha ripoti kwenye bodi ya magavana wa shirika hilo.

Bwana Amano amewataarifu nchi wanachama kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ukaguzi wa nyuklia nchini Iran na Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea. Ameeleza hatua zilizopigwa katika utekelezaji wa mpango wa IAEA wa usalama wa nyuklia akitolea mfano mtazamo wa karibuni wa kimataifa kuhusu maendeleo ya nguvu za nyuklia.

Pia bwana Amano ametaja pendekezo la mradi mpya wenye lengo la kuimarisha uwezo wa kanda ya Afrika katika kuchunguza magonjwa ya kuambukiza ya wanyama kama vile Ebola ambayo inaweza kuambukizwa kwa binadamu.

Bodi hiyo ambayo hukutana mara tano kwa mwaka kwenye makao makuu ya IAEA mjini Vienna Austria ni moja ya vyombo vikuu vya kutunga sera katika shirika hilo.