Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama laangazia ulinzi wa wanawake vitani

Baraza la usalama laangazia ulinzi wa wanawake vitani

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu ulinzi wa raia katika vita, mjadala uliojikita zaidi katika ulinzi dhidi ya wanawake vitani. Abdullahi Boru na maelezo kamili.

(TAARIFA YA ABDULLAHI)

Akiongea katika mjadala huoMsaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu misaada ya kibinadamu Kyung-Wha Kang amesema ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake katika mizozo bado unaendelea akitolea mfano Syria na Nigeria.

(SAUTI KANG)

"Katika baadhi ya maeneo pande kinzani kwa makusudi zinalenga raia na kutumia mbinu za kusababaisha madhara kubwa. Nchini Nigeria Boko Haram imewaua mamia ya raia na kuteketeza maelfu ya nyumba, shule na hospitali katika wiki chache zilizopita na haya yanafuatia matukio ya mara kwa mara ya utekaji nyara wa mamia ya wanawake na watoto. Nchini Syria na Iraq pande zote zimeshambulia raia kwa misingi ya ukabila na udini."

Kwa upande wao wawakilishi wa nchi na taasisi mbalimbali za haki za binadmau wamesema lazima hatua za lazima zichukuliwe kulinda raia hususani wanawake katika maeneo ya vita na kutaka pande kinzani kuruhusu misaada iwafikie waathirika katika maeneo husika.