Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yajitahidi kuokoa wafanyakazi wake Sudan

WFP yajitahidi kuokoa wafanyakazi wake Sudan

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linaendelea na jitihada zake ili wafanyakazi wake sita wanaoshikiliwa huko eneo la Kordofan Kusini nchini Sudan waweze kuachiliwa huru.

Wafanyakazi hao ni wa helikopta ya Umoja wa Mataifa ambayo ilikuwa inasafiri kutoka Sudan Kusini kwenda Khartoum nchini Sudan kwa ajili ya matengenezo ya kawaida siku ya Jumatatu lakini ilifanya kituo cha dharura Kordofan Kusini na yadaiwa wanashikiliwa na waasi wa Sudan People's Liberation Movement, SPLM-North.

George Fominyen, Afisa habari wa WFP amethibitisha kuwa wafanyakazi hao wako hai alipozungumza na Radio Miraya.

(Sauti ya George)

“Tumepata taarifa ya kwamba wafanyakazi hao wako hai lakini sasa tunajitahidi ili tuweze kuzungumza nao moja kwa moja na pia tunajitahidi ili waweze kuachiliwa huru haraka na salama.”

Waasi wa SPLM-North wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya Sudan tangu mwaka 2011.