Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kushuka kwa bei ya mafuta kichocheo cha ukuaji wa uchumi:Ripoti

Kushuka kwa bei ya mafuta kichocheo cha ukuaji wa uchumi:Ripoti

Ripoti mpya kuhusu matarajio ya ukuwuaji wa uchumi duniani ya Benki ya Dunia iliyotolewa hivi leo imesema kufuatia mwaka mwingine wa kukatisha tamaa, nchi zinazoendelea zitashuhudia  ukuaji wa kiuchumi mwaka huu, chachu ikiwa ni kushuka kwa bei ya mafuta ya petroli, ukuaji imara wa uchumi wa Marekani, na viwango vya chini vya riba duniani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baada ya kuongezeka kwa wastani ya asilimia 2.6 mwaka 2014, uchumi wa dunia unatarajiwa kukua kwa asilimia 3 mwaka huu, asilimia 3.3 mwaka ujao na asilimia 3.2 mwaka 2017.

Mwaka wa 2014, nchi zinazoendelea zilikuwa kwa asilimia 4.4, lakini mwaka huu zinatarajiwa kuwa kwa asilimia 4.8 na kutabiriwa kukua kwa  asilimia 5.3 na 5.4 mwaka 2016 na 2017 mtawalia.

Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim amesema katika mazingira haya ya kubadilika badilika, nchi zinazoendelea zinahitaji kutumia raslimali zake kwa busara katika kuwekeza kwenye miradi ya kijamii kwa kuzingatia watu masikini na kufanya mageuzi ya kimuundo inayowekeza kwa watu.

Ayhan Kose, Mkurugenzi katika Benki ya Dunia.

 “Hatari ya ahueni hii tete bado ni kubwa. Benki Kuu katika nchi zinazoendelea zinahitaji kuleta usawa kati ya kulenga ukuaji wa kiuchumi na kulenga mfumuko wa bei na utulivu wa fedha. Wakati huo huo, sera ya fedha inaweza kuwa chombo cha kuchochea ukuaji wa uchumi wao, iwapo kutakuwepo na mtikisiko wa kiuchumi."