Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sierra Leone kinara wa visa vya Ebola: WHO

Sierra Leone kinara wa visa vya Ebola: WHO

Shirika la afya ulimweguni WHO linasema Sierra Leone ndiyo nchi iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa wa homa kali ya Ebola.

Mkuu wa WHO Margaret Chan anasema mamia ya visa vinaripotiwa kila juma nchini humo ambapo visa 248 vilithibitishwa katika juma la kwanza la mwezi January.

Hata hivyo idadi ya visa imeanza kupungua ikilinagnishwa na awali.

WHO inasema kuwa nchini Liberia visa vya Ebola vimepungua katika wilaya 12 kati ya 15 kandoni mwa wilaya ya Montserrado inayoongoza kwa idadi ya visa nchini humo.

Wakati huohuo takwimu zinaonyesha kuwa nchini Guinea kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mlipuko wa Ebola nchi hiyo imethibitisha rikodi ya visa 160.

Takwimu hizi zinakuja wakati ambapo mkutano mkuu kuhusu kinga ya homa kali ya Ebola na uwezeshaji wa kifedha ukiendelea mjini Geneva.

Ugonjwa huo umegarimu vifo vya watu zaidi ya 8,000 wengi wao wakiwa ni katika nchi tatu, Liberia, Sierra Leone na Guiena