Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICAO Yapendekezo mpango mpya wa Usalama wa usafiri wa ndege

ICAO Yapendekezo mpango mpya wa Usalama wa usafiri wa ndege

Shirika la kimataifa la usalama wa anga, ICAO limependekeza mpango mpya wa kufuatilia ndege zilizopo nje ya mtambo wa mawasiliano-ya rada wakati wanaporuka juu ya bahari. Pendekezo hilo la ndege lianata ndege kutoa taarifa kila baada ya kila dakika 15 na linakuja baada ya kupotea kwa ndegea ya shirika la Malaysia Airline katika bahari ya Hindi mwezi Machi mwaka jana.

Mkuu wa Usalama wa ICAO John Illson anaelezea pendekezo hilo

(SAUTI JOHN)

"Kuna mabadiliko mengine yanayozingatiwa na mabadiliko hayo ni ya muda mrefu na yanahusu mabadiliko ya ujumla ya vifaa, ndege au sehemu nyingine za mifumo. Pendekezo la ICAO la muda mfupi, ni lile ambalo halihitaji mabadiliko ya vifaa na yanaweza kutekelezwa kwa haraka sana."