Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majaribio ya chanjo dhidi ya Ebola kufanyika punde: WHO

Majaribio ya chanjo dhidi ya Ebola kufanyika punde: WHO

Majaribio ya chanjo dhidi ya kinga ya homa kali ya Ebola yanatarajiwa kufanyika mwezi huu na mwezi ujao katika nchi zilizoathiriwa zaidi Afrika Magharibi. Amina Hassan na maelezo kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Hatua hii inafuatia mkutano unaoendelea chini ya shirika la afya ulimwenguni WHO mjini Geneva ambapo washiriki wamesema wanataka dawa mpya itolewe haraka iwezekanavyo.

Hatua hii inafuatia mkutano unaoendelea chini ya shirika la afya ulimwenguni WHO mjini Geneva ambapo washiriki wamesema wanataka dawa mpya itolewe haraka iwezekanavyo.

Profesa  Helen Rees ni Dk kutoka WHO

(SAUTI REES)

"Bado hatujapata chanjo ya uhakika kwa sasa.... kile tunachokusudia ni kufanya haraka iwezekanavyo ni kuchukua fursa hii ya kutengeneza chanjo ya hali ya juu wakati janga hili likiendelea  chanjo ambayo itaweza kukabiliana na hali ya saa, tukizingatia kwamba tungalikuwa na muda mwingi tungalifanya mambo mengi zaidi kabla ya kutumia chanjo katika kliniki, hatuna fursa hiyo, tunachosema ni kwamba kile tumekiona kinaleta matumaini na ni vizuri tuanze kuitumia haraka iwezekanavyo."

Kwa mujibu wa WHO, Liberia itakuwa nchi ya kwanza kufanyiwa majaribio ya chanjo mbili dhidi ya Ebola mwishoni mwa mwezi huu huku majaribio ya chanjo nchini Sierra Leone na Guinea  yakitarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

Shirika hilo limesema inachukua hadi  miezi sita kuona ikiwa chajo dhidi ya Ebola inafanya kazi baada ya majaribio kwa maelfu wa watu.