Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uturuki yapongezwa kwa juhudi zake za kupambana na majanga

Uturuki yapongezwa kwa juhudi zake za kupambana na majanga

Uturuki imesifiwa kama kiongozi katika kupunguza majanga hatari miaka mitano baada ya kuunda mamlaka ya kimataifa ya usimamizi wa dharura, AFAD iliyoko chini ya udhibiti wa moja kwa moja ya Ofisi ya Waziri Mkuu.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye utekelezaji wa mkakati wa kupunguza athari za majanga , Bi Margareta Wahlström, amesema kuundwa kwa AFAD miaka mitano ilyopita ni kitendo cha ujasiri kwa kuwa ilitambua ukweli kwamba kufanikiwa kwa sera inhitaji taasisi imara za kuhakikisha utekelezaji wa sera zenyewe.

Wahlström amesema Uturuki ni mojawapo ya taifa linalokabiliwa na majanga lakini pia imekuwa na historia ya muda mrefu ya usimamazi wa majanga hayo hatari, kwa maantiki hiyo kwa kuundwa kwa AFAD ni dhirisho tosha ya mabadiliko ya kimkakati katika usimamazi wa majanga kwa kuangazia uwezo wa taasisi.

Aidha, katika ujumbe wake kwa AFAD , Bi Wahlström amepongeza uongozi wa Uturuki katika uzinduzi wa Mpango wa Shule Salama kote duniani ambayo itakuwa mojawapo ya kipengele katika ajenda ya Mkutano wa Tatu ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza Majanga Hatari itakayofanyika mwezi Machi mjini Sendai nchini Japan.