Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio kwenye arusi nchini Afghanistan

Ban alaani shambulio kwenye arusi nchini Afghanistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelani vikali shambulio kwenye sherehe ya arusi katika jimbo la Helmand nchini Afghanistan hapo jana lililosababisha vifo vay  raia 25 huku watu  45 wakijeruhiwa vibaya.

Taarifa ya Ban kupitia msemaji wake imemnukuu Katibu Mkuu akihimiza serikali kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria.

Kadhalika Bwana Ban ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga huku akiwatakia afueni ya haraka majeruhi.