Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP na washirika wazindua changizo la chakula kwa nchi zilizoathiriwa na Ebola

Msaada wa chakula utasaidia wakati wa quarantini katika nchi zinazokabiliana na ebola.(Picha ya WFP)

WFP na washirika wazindua changizo la chakula kwa nchi zilizoathiriwa na Ebola

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula , WFP na washirika leo wamezindua uchangishaji wa fedha kwa ajili ya usaidizi wa chakula kwa familia ambazo zimeathiriwa na mlipuko wa homa kaliya Ebola Afrika magharibi.

Liberia na Sierra Leone ni miongoni mwa nchi hizo ambapo takribani watu 500,000 wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula.

WFP na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO hivi karibuni yalionya kuwa takribani watu milioni moja wanaweza kuachwa bila chakula nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia.

Stephane Dujarric ni msemaji wa Umoja wa Mataifa

"Shirika la mpango wa chakula (WFP) na taasisi ya China ya  kushughulikia msuala ya umasikini CFPA) yanazindua leo changizo la kijamii kwa kushirikiana na kampuni kubwa duniani ya internet iitwayo Tencent.Fedha zitakazochangishwa zitaelekezwa kwenye operesheni za dharura za WFP  ili kusaidia mahitaji ya chakula na mahitaji mengine ya msingi kwa familia na jamii zilizoathiriwa katika nchi tatu zilizoathiriwa zaidi ambazo ni Ebola –Sierra Leone, Liberia and Guinea."

Amesema tangu mlipuko wa Ebola mwezi April, WFP imetoa msaada wa chakula kwa zaidi ya watu milioni 2.

Mashirika hayo ya masuala ya chukula pia yametoa misaada ya madawa kwa kuwezesha usafiri kwa jamii ikiwamo usafiri wa anga kwa watu na chakula.