Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujerumani yatambua umuhimu wa mfumo wa tahadhari ya Tsunami

Picha@UNESCO

Ujerumani yatambua umuhimu wa mfumo wa tahadhari ya Tsunami

Ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Serikali ya Ujerumani umepata msukumo mpya baada ya Ujerumani kupitia Wizara yake ya Uchumi na Maendeleo kutoa kiasi cha euro 250,000 kwa ajili ya kuendeleza mfumo wa tahadhari ya mapema katika maeneo ya pwani.

Kiasi hicho cha fedha kilichotolewa kwa Kamishna ya UN inayohusika na uchumi na ustawi wa kijamii kwa Asia ni sehemu ya mkakati wa kutunisha mfuko wa Tsunami.

 Fedha hizo ni mwendelezo wa michango ya Ujerumani kwa kamishna hiyo baada ya kutoa kiasi kingine cha fedha cha euro 500,000 mwezi disemba mwaka jana.