Liberia yafanya uchaguzi licha ya mlipuko wa ebola

Shughuli za uchaguzi nchini Liberia(Picha ya UM/videocapture/Unifeed)

Liberia yafanya uchaguzi licha ya mlipuko wa ebola

Kamanda Mkuu wa vikosi vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia  UNMIL, Meja Jenerali Leonard Ngondi amesema uamuzi wa mahakama kuu ya Liberia kuamua uchuguzi wa maseneta kufanyaik Desemba 20 nchini humo  umetoa uwazi kwa wananchi wakati wa uchaguzi.

Katika mahojiano na idhaa hii kuhusu uchaguzi huo ambao umefanyika mwishoni mwa juma Bwana Ngondi amesema uwezekano wa uchaguzi wa amani wakati huu mgumu ni ishara ya demokrasia endelevu nchini Liberia.

(sauti ya Ngondi)

Kadhalika Meja Jenerali Ngondi akasema kwamba wakati wa uchaguzi tahadhari ilichukiliwa ili kuzuia maambukizi ya homa kali ya Ebola.

(sauti ya Ngondi)