Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za kusaka uzao zatishia uhai na ustawi wa mtoto

Mtoto aliyeokolewa akishuhudia mama yake (upande wa kushoto) akimshukuru msamaria mwema. (Picha:John Kibego, Spice FM)

Harakati za kusaka uzao zatishia uhai na ustawi wa mtoto

Mizozo na sintofahamu katika baadhi ya familia imekuwa mwiba kwa watoto ambao  hujikuta katika mazingira ambayo hawakutarajia halikadhalika wazazi wao. Hali hii imejiri kwa mtoto mmoja wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye alijikuta kwenye mikono ya mwanamke asiye mama yake mzazi kutokana na mama huyo kuhaha kusaka mtoto na hivyo kutishia uhai na ustawi wa mtoto huyo. Je nini kilijiri? Tuungane basi na John Kibego wa radio washirika ya Spice Fm nchini Uganda.