Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumepiga hatua , juhudi zaidi zahitajika: Nabarro

UN Photo/Marlon Lopez
Picha:

Tumepiga hatua , juhudi zaidi zahitajika: Nabarro

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola UNMEER  David Nabarro amesema malengo ya maziko salama ya asilimia 70 kwa vifo vitokanavyo na Ebola yamefanikiwa lakini utoaji tiba kwa asilimia hiyo bado ni changamoto. Taarifa kamili na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Akizungumza katika mkutano na waaandishi wa habari hii leo katika kituo cha kitaifa cha kushughulikia Ebola  nchini Sierra Leone Nabarro amesema mchango mkubwa wa jumuiya ya kimataifa unahitajika ili kutokomeza maaambukizi

(Sauti ya Nabbaro)

“Hatua zinapaswa kubadilishwa kadri mlipuko unavyotokea. Pale ambako kasi ya ugonjwa ni kubwa , msisitizo ni katika uhamasishaji jamii, mazishi salama na huduma muhimu kwa wahitaji. Yote hayo ni muhimu sana iwapo kasi ya hatua zinazochukuliwa ni ndogo kuliko ile ya mlipuko.”

Katika hatua nyingine UNMEEER imesema hakuna kisa kipya cha Ebola kilichoripotiwa nchini Mali. UNMEER imemkariri Rais wa  nchi hiyo Boubacar Keita ambaye amesema mwishoni  mwa juma kuwa  taifa hilo la Magharibi mwa Afrika halina kisa kipya na hivyo hadi sasa idadi ya waliofariki kwa Ebola inasalia  kuwa watu saba