Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muhogo na Samaki vyabadili maisha ya wakazi wa Tanzania

Uvuvi wa samaki katika ziwa Victoria. Picha kutoka video ya UNIFEED.

Muhogo na Samaki vyabadili maisha ya wakazi wa Tanzania

Tarehe 20 Novemba kila mwaka ni siku ya maendeleo ya viwanda barani Afrika. Siku hii iliidhinishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1989 kwa lengo la kuangazia viwanda kama moja ya sekta muhimu za kuchagiza maendeleo barani humo. Mwaka huu ujumbe umejikita katika kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi za kilimo katika eneo husika. Je kulikoni basi ungana na Joseph Msami kwenye makala hii.