Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi 13 kutuzwa kwa juhudi za kukabiliana na njaa

Picha:FAO

Nchi 13 kutuzwa kwa juhudi za kukabiliana na njaa

Nchi kumi na tatu zitapokea tuzo la Shirika la Chakula na Kilimom, FAO, kufuatia hatua zilizopiga katika kukabiliana na njaa.

Brazil, Cameroon, Ethiopia, Gabon, The Gambia, Iran, Kiribati, Malaysia, Mauritania, Mauritius, Mexico, Ufilipino na Uruguay ndizo nchi ambazo zimetambuliwa na FAO kwa juhudi za kukabiliana na tatizo la lishe duni. Pamoja na kufikia lengo la maendeleo ya milenia la kupunguza kwa nusu idadi ya watu wenye njaa ifikapo mwaka 2015, nchi hizo pia zimetimiza lengo la mkutano wa kimataifa kuhusu chakula wa mwaka 1996, la kupunguza watu wenye njaa iliyokithiri kwa nusu ifikapo mwaka 2015.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO, José Graziano da Silva, atatambua juhudi za nchi hizo kwa kuwakabidhi wawakilishi wao tunu za diploma kwenye hafla iliyopangwa kufanyika kwenye makao makuu ya FAO mjini Roma, Italia, mnamo Novemba 30, 2014.