Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pikipiki zazindua siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

Wahamasishaji wa pikipiki kambi ya Kyangwali. Picha ya John Kibego

Pikipiki zazindua siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

Nchini Uganda, pikipiki za bodaboda zimetumiwa kuzindua rasmi siku 16 za uanaharakati wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake, katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali magharibi mwa nchi. John Kibego wa radio washirika ya Spice fm nchini humo, ameshuhudia shamra shamra za uzinduzi.

(Tarifa ya John ibego)

Ni pikipiki za wakimbizi wakizunguka kambi hii wakiwambia jamii kwamba kampeni imeanza. Baadaye wadau tofauti walikusanyika kwenye shule ya msingi ya Kasonga na kampeni ikazinduliwa rasmi.

Johansen Kasenese, afisa wa huduma za jamii wa kambi hii amezungumzia baadhi ya vitakavyofanywa

(Sauti ya Johansene Kasenene)