Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa uhifadhi wa tamaduni wafanyika Geneva

Utamaduni kutoka Kenya, Uganda na Venezuela watajwa katika orodha ya uhifadhi.(Picha ya UNESCO)

Mkutano wa uhifadhi wa tamaduni wafanyika Geneva

Utamduni wa utakaso wa watoto wa kabila la Lango lililoko nchini Uganda ni moja ya tamaduni zinazotarajiwa kulindwa na kuhifadhiwa ikiwa ni matokeo ya mkutano kuhusu uhifadhi wa tamaduni mjini Geneva Uswis.

Mkutano huo  wa tisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO  unaoangalia tamaduni zilizoko hatarini kutoweka unaendelea Geneva, Uswizi unahusisha mataifa 24 yaliyoteuliwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa katika makataba wa mwaka 2003 kuhusu mkataba wa uhifadhi wa urithi wa utamaduni utaangazia maeneo nane yaliyopendekezwa kwa ajili ya kulindwa .

Miongoni mwa tamaduni zilizoorodheshwa katika orodha ya uhifadhi ni pamoja na ngoma ya koo za  Ishuka na Idhako  kutoka nchini Kenya .