Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutesa aisifu kazi ya Baraza la Haki za Binadamu

UN Photo/Devra Berkowitz
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Sam Kutesa,(

Kutesa aisifu kazi ya Baraza la Haki za Binadamu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limesikiliza ripoti ya kila mwaka ya Baraza la Haki za Binadamu, ambayo imewasilishwa na Rais wa Baraza la Haki za Binadamu, Baudelaire Ndong Ella.

Akizungumza kabla kumkaribisha Bwana Ndong Ella kutoa ripoti hiyo, Rais wa Baraza Kuu, Sam Kutesa, amesisitiza umuhimu wa Baraza la Haki za Binadamu

“Kwa kukabiliana na ukiukaji wa haki za binadamu, Baraza hilo lina jukumu muhimu la kuendeleza heshima ya haki za binadamu na uhuru wa kila mmoja kila mahali. Na katika hili, kazi ya Baraza hilo ya na kupambana kwa bidii na kwa njia endelevu dhidi ya hali za ukiukaji wa haki za bindamu duniani ni ya kupongezwa.”

Bwana Kutesa ameorodhesha baadhi ya masuala ambayo Baraza hilo limefanikiwa kushghulikia

“Baraza hilo halijaweza tu kukabiliana na masuala ya nchi binafsi, lakini limejikita sana pia katika kuendeleza uwanja mzima wa haki za binadamu, zikiwemo haki za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni, na haki ya maendeleo. Baraza hilo limewapa walio wanyonge zaidi sauti na wale walio hatarini kubaguliwa na kunyimwa haki zao za binadamu.”