Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa wa kudhibiti silaha ni ushindi mkubwa: Ban

Kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa wa kudhibiti silaha ni ushindi mkubwa: Ban

Kitendo cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha mkataba wa kimataifa wa kudhibiti biashara ya silaha, ATT ni ushindi wa dunia nzima na hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon. Katika ujumbe wake, Bwana Ban amesema sasa itakuwa vigumu kwa soko haramu la silaha kushamiri duniani na kwamba wababe wa kivita, maharamia, magaidi na wahalifu watashindwa kupata silaha hizo kirahisi. Amesifu hatua za nchi wanachama kulegeza misimamoyaokwa maslahi ya haki za binadamu, amani na utulivu duniani pamoja na ushiriki wa mashirika ya kiraia tangu kuanzishwa kwa mchakato wa kupatikana kwa nyaraka hiyo. Katibu Mkuu amesema kitendo cha leo kimedhihirisha vile ambavyo mambo makubwa yanaweza kuafikiwa pindi serikali na vikundi vya kiraia vinaposhirikiana kupitia Umoja wa Mataifa. Bwana Ban amesema Umoja  wa Mataifa kwa upande wake utatoa usaidizi wote unaohitajika ili mkataba huo uweze kufanikiwa.