Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana waomba kushirikishwa zaidi katika utungaji sera: mjumbe wa Kenya

vijana waliojadili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa pamoja na Katibu Mkuu Ban Ki Moon. Picha ya UN, Mark Garten.

Vijana waomba kushirikishwa zaidi katika utungaji sera: mjumbe wa Kenya

Kamati ya tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kijami, kibinadamu na kitamaduni imehitimisha mjadala mkuu kuhusu maendeleo ya kijamii kwa kusikiliza maoni ya vijana kutoka duniani kote. Wengi wameomba kushirikishwa zaidi katika utungaji sera.

Miongoni mwao, Wambui Kahara, mwakilishi wa vijana nchini Kenya, amesema malengo ya milenia hayaeleweki kwa vijana wengi nchini Kenya hasa vijijini, lakini ni muhimu wawezeshwe ili kushiriki zaidi kwenye maswala hayo ambayo yanawahusu.

Amesema serikali ya Kenya imejitahidi kuwapa vijana nafasi zaidi, hasa kupitia sheria mpya ya zabuni ambayo inawapatia vijana asilimia 30 ya zabuni zote za serikali.

(Sauti ya Wambui)