Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya migogoro elimu yapigiwa upatu nchini Syria

Adnan, mtoto wa miaka mitano aliyejehuriwa wakati wa mashambulizi nchini Syria. Picha ya UNICEF/Marta Ramoneda

Licha ya migogoro elimu yapigiwa upatu nchini Syria

Hebu fikiria kupata elimu katikati ya mtutu wa bunduki na milio ya mabomu. Ndivyo ilivyo nchini Syria ambapo wakati mzozo ukiendelea jmuiya ya kimataifa kwa kushirikiana na mamalaka za nchi hiyo zinahaha kunusuru elimu ya msingi Syria.

Ungana na Joseph Msami anayesimulia kile kinachojiri katika kusongesha juhudi za elimu katika nchi ambayo imetumbukia kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.