Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuzingatie wito wa Mahatma Gandhi wa kusaka amani bila vurugu: UM

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon alipotembea kaburi la Mahatma Gandhi lililoko eneo la Raj Ghat nchini India mwaka 2008. (picha:UN/Mark Garten)

Tuzingatie wito wa Mahatma Gandhi wa kusaka amani bila vurugu: UM

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Jan Eliasson wamekuwa miongoni viongozi waandamizi waliohutubia kwenye tukio maalum la kukumbuka kuzaliwa kwa mwanaharakati na Baba wa Taifa laIndia, Mahatma Gandhi lililofanyika mjiniNew York.

Tukiohiloliliandaliwa naIndiakatika siku ambayo Umoja wa Mataifa inaitambua kuwa ni siku ya kupinga vurugu na ukatili kwa kuzingatia hulka ya Mahatma Gandhi ya kudai haki bila kutumia ghasia.

Bwana Kutesa akatumia fursa hiyo kueleza kuwa kwa sasa mizozo mingi inaibuka na kuenea duniani akitaja wanamgambo wanaotaka kuunda dola la kiislamu hukoIraqnaSyriakamamoja ya mfano na hivyo kutaka hatua zaidi zichukuliwe kudhibiti vitendo hivyo.

(Sauti ya Kutesa)

“Tumeshuhudia ongezeko la mizozo ya mapigano duniani kote, wakati kuna vitisho vingine vinavyotekelezwa na magaidi na watu wenye misimamo mikali vinabadili misingi ya amani na  usalama duniani. Hivyo sasa kuliko wakati wote, jamii ya kimataifa lazima iimarishe jitihada zake za kutatua mizozo kwa njia ya amani.”

(Sauti ya Eliasson)

Naibu Katibu Mkuu Eliasson katika hotuba yake amesema mizozo mingi inaendelea duniani na mara nyingi hatua zinazochukuliwa kukabiliana nayo ni vurugu zaidi ilhali kinachotakiwa ni majadiliano na maridhiano.

“Kwa hiyo ni wakati muafaka kurejelea wito wa Mahatma Gandhi wa kusaka amani bila vurugu. Ni lazima tukatae kuwa vurugu ni njia ya kawaida ya kuleta amani. Ni lazima tuzingatie njia ya kusaka amani bila vurugu na kusuluhishi mizozo kwa amani kama mwelekeo wa mabadiliko endelevu ya jamii zetu.”