Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yaahidi kupanda miti milioni 2.5 kila mwaka

Upandaji wa miti nchini Uganda. Picha ya UNHCR/Dorothy

Uganda yaahidi kupanda miti milioni 2.5 kila mwaka

Baada ya hotuba ya rais wa Uganda Yoweri Museveni katika Mkutano wa viongozi wa nchi na serikali kuhusu mabadiliko ya tabianchi, Mkuu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika wizara ya Maji na Mazingira ya Uganda, Chebet Maikut, amefafanua zaidi kuhusu ahadi zilizotangazwa na rais wa Uganda, akiongea na Idhaa hii katika ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.