Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za visiwa vidogo kujadili maendeleo nchini Samoa

Picha@UN

Nchi za visiwa vidogo kujadili maendeleo nchini Samoa

Wakati mkutano wa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea  (SIDS) ukitarajiwa kuanza tarehe Mosi mwezi ujao hukoSamoa,  nchi hizo zinatarajiwa kutumia mkutano huo kuifikia jumuiya ya kimataifa kwa ajili ya misaada.

Miongoni mwa mada zitakazojadiliwa ni mabadiliko ya tabia nchi, maendeleo endelevu na kukabiliana na majanga. Ali'ioaiga Feturi Elisaia ambaye ni ni mwakilishi wa kudumu wa Samoa katika Umoja wa Mataifa anazungumzia fursa muhimu katika mkutano huu.

(SAUTI ELISAIA)

 "Tunawafikia washirika wa maendeleo . Tunaufikia Umoja wa Mataifa kwa kutumia mtandao wake wa kimataifa ili ujumbe ufike kwa walengwa katika mijini ambapo maamuzi mengi hufanyika."

Hii ni mara ya tatu jumuiya ya kimataifa inakutana kujadili ukuaji wa nchi hizi huku pia utekelezaji wa maendeleo ya milenia ukitarajiwa kuangaziwa.