Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa MONUSCO atembelea “visiwa vya amani” magharibi mwa DRC

Martin Kobler mkuu wa MONUSCO akizungumza na wanafunzi kwenye kijiji cha Kivu Kaskazini, @MONUSCO/SylvainLiechti

Mkuu wa MONUSCO atembelea “visiwa vya amani” magharibi mwa DRC

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, MONUSCO, Martin Kobler, ameanza ziara maalum ya kutembelea visiwa vya amani mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa MONUSCO, visiwa vya amani ni sehemu maalum zilizopata amani baada ya miaka mengi ya mapigano, ambapo MONUSCO inajaribu kutengeneza hali ya utulivu endelevu kwa kuzingatia jitihada na misaada yake.

Dona Mabimba mwandishi wa habari kutoka Radio washirika OKAPI huko DR Kongo anafafanua.

(Sauti ya mwandishi wa Radio Okapi)

“ Baada ya kushinda kundi la waasi la M23 na mapigano dhidi ya waasi wengine DRC, MONUSCO imeamua kusambaza mradi huo wa visiwa vya amani kwa kuondoa wanamgambo wote kwenye eneo maalum, kurejesha amani, kurudisha hali ya maisha ya kawaidia, na kuimarisha mamlaka za serikali. Hayo yanaendelea kwenye baadhi ya maeneo ya DRC, kama vile Masisi ama Sange, Kivu Kusini au Walikale, Kivu Kaskazini, ambako tayari ni visiwa vya amani kwa mujibu wa MONUSCO. Ndiyo maana mkuu wa MONUSCO Martin Kobler ametembelea baadhi ya visiwa hivyo mashariki mwa nchi”