Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU na UN Women watangaza tuzo mpya ya teknolojia na usawa wa jinsia

ITU

ITU na UN Women watangaza tuzo mpya ya teknolojia na usawa wa jinsia

Shirika la Kimataifa la Mawasiliano, ITU na lile la masuala ya wanawake, UN Women, kwa pamoja yametangaza kuanzisha tuzo mpya ya kimataifa kwa ajili ya kutambua juhudi bora  zaidi katika kutumia teknolojia ya mawasiliano (ICT) kuendeleza usawa wa jinsia.

Tuzo ya GEM-TECH, itawatambua viongozi na mashirika yanayotumia uwezo wa teknolojia kuleta mabadiliko. Tuzo hiyo itatolewa kwa washindi saba wa kiserikali, sekta binafsi, wasomi na mashirika ya umma, kwenye kongamano la ITU, ambalo litafanyika mjiniBusan,Korea, kuanzia tarehe 20 Oktoba hadi tarehe 7 Novemba.

Washindi watasafiri kwenda Busan kupokea tuzo zao, na kuiunga kwa hafla ya kimataifa ya tarehe 21 Oktoba, inayolenga kupigia debe uwezo wa ICT katika kubadilisha maisha. Uteuzi wa wagombea wa tuzo hiyo utafunguliwa mnamo Septemba 5, 2014 kwenye tovuti www.itu.int/gem-tech-awards.