Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka vyuo vikuu kusaidia kuwawezesha wanawake

Ban ataka vyuo vikuu kusaidia kuwawezesha wanawake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa katika mataifa mengi wanawake wameendelea kuchukuliwa kama watu wa daraja la pili hivyo ametoa wito kwa vyuo vikuu kuweka msukumo wa kubadilisha mwenendo huu aliouita wa kibaguzi.

Amesema wasomi wana nafasi kubwa ya kubadilisha dhana hizo potofu ambazo zinawarudisha nyuma wanawake wangi kwa kuwapa alama kwamba wahawezi kufanya mazuri ya mafanikio.

Akizungumza kwenye mhadhara wa kimataifa uliofanyika kwenye chuo kikuu cha Pennsylvania Ban ameongeza kusema kuwa vyuo vikuu vinanafasi kubwa ya kusaidia kuvunja tabata hilo la kupalilia usawa wa kijinsia.

Amesema wasomi wanachukua fursa ya pekee ya utoaji elimu na mafunzo ambayo yanaweza kuhamasisha mitazamo mipya kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo ya ujenzi wa demokrasia.