Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la kimataifa la watu wa asili limemalizika mjini New York kwenye UM

Kongamano la kimataifa la watu wa asili limemalizika mjini New York kwenye UM

Kongamano la kimataifa kuhusu watu wa asili lililokuwa likiendelea kwenye makao makuu ya UM New York limemalizika leo.

Uhusiano baiana ya watu hao na misitu ilikuwa moja ya ajenda zilizojadiliwa huku washiriki wakielezea hofu yao juu ya athari za ukataji misitu , uchimbaji madini na miradi mikuwa ya ujenzi kwao na maisha yao. Pia washirikia wametaja hofu juu ya vitendo ya watu hao wa asili kuendelea kuondolewa kwa nguvu kutoka misituni kwao.

Mwenyekiti wa zamani wa kongamano hilo Tauli Coropuz amesema hilo ni swala nyeti kwa watu wa asili. Amesema watu hawa wanaondolewa kwa nguvu watu kutokana na ujenzi wa miradi kama uchimbaji mafuta, hifadhi za wanyama na ujenzi wa viwanda.