Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango mpya wazinduliwa kukabiliana na ukatili wa kingono

Picha@UNICEF

Mpango mpya wazinduliwa kukabiliana na ukatili wa kingono

Nchini Tanzania, msichana mmoja kati ya watatu hukabiliana na ukatili wa kingono kabla hajafikisha miaka kumi na minane. Bado desturi ya siri inakuwepo na kusababisha watekelezaji wengi kukwepa sheria. Ili kudhibiti ukatili huo, serikali ya Tanzania imezindua mpango mpya wa miaka mitatu wa kuripoti ukatili wa kingono kwa kupitia madawati ya jinsia na watoto yanayofunguliwa katika kila wilaya.

Je, mpango huo unafanikiwa? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.