Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Linda Lango fikia lengo: UNAIDS yanena huko Brazil

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Mkurugeniz Mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe kwenye moja ya kampeni hizo. Picha@UN/ Eskinder Debebe)

Linda Lango fikia lengo: UNAIDS yanena huko Brazil

Wakati michuano ya Kombe la Dunia ikianza rasmi hii leo nchini Brazil, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na suala la HIV na Ukimwi, UNAIDS, limehamishia huko kampeni yake ya kulinda lengo la milenia kuhusu kupunguza maambukizi ya HIV. Taarifa kamili na Amina Hassan

Taarifa ya Amina Hassan

Kampeni hiyo hutumia nguvu za michezo za kuwaleta watu pamoja kuwawezesha vijana kupata huduma za kuzuia, na matibabu dhidi ya HIV.

Tayari kumefanyika hafla ya kampeni hiyo kwenye ukumbi wa Castro Alves katika jimbo la Salvador nchini Brazil, ambako Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS, Michel Sidibé amesema mchezo wa kandanda ni wa kipekee kwa jinsi unavyowaunganisha watu kutoka sekta zote za jamii, kwa msisimko mmoja.

Lengo la kampeni hiyo ni kutumia msisimko unaoletwa na Kombe la Dunia kuongeza juhudi za kuhakikisha kwamba vijana wanajilinda dhidi ya HIV na kupata huduma za kuokoa maisha kutokana na HIV.

Tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekwenda Brazil kuhudhuria halfa ya ufunguzi wa michuano hiyo