Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Monusco yaalani kuzuka kwa mapigano ya kikabila mjini Uvira-Mkoa wa Kivu Kusini- DRC

Martin Kobler@UN

Monusco yaalani kuzuka kwa mapigano ya kikabila mjini Uvira-Mkoa wa Kivu Kusini- DRC

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambaye pia ni  mkuu wa MONUSCO, Martin Kobler ameshutumu vikali mapigano yaliyotokea ijumaa iliyopita  baina ya jamii ya Bafuliru na Burindi na ile ya Banyamulenge ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 30 na majeruhi 15 katika sehemu hiyo.

Mkuu huyo wa MONUSCO amesema kwamba mapigano hayo yasitishwe mara moja ili kurejesha amani na utuliviu kwenye eneohilo.

Kufifikia sasa, Jeshi  la kulinda amani la Umoja wa Mataifaa na Jeshi la serikali ya Demokrasia ya Congo FARDC wanashirkiana kukomehsa ghasia na kuwahamisha waathiriwa ili wapate matibabu kwenye zahanati zilizoko karibu.

Wanajeshi wa kulinda amani wameweka doria katika wilaya ya Mutarule  ili kuimarisha hali ya amani wakisaidiana na Jeshi la Serikali ya DRC kudhibiti hali hiyo, na kuwalinda raia.

Imebainika kuwa mapigano hayo yalisababishwa na wizi wa mifugo katika mji wa Ruzizi kilomita 40 Kaskazini mwa  Uvira,  sehemu ambayo ilikumbwa zaidi na mapigano hayo.