Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yahitaji fedha zaidi kunusuru mahitaji ya chakula CAR

WFP yahitaji fedha zaidi kunusuru mahitaji ya chakula CAR

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema linakabiliwa na upungufu wa fedha kwa ajili ya kugawa mahitaji ya chakula nchini jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.

Shirika hilo linasema ili kuepuka kugawa nusu chakula kwa walengwa au kuahirisha kabisa ahadi zaidi za fedha zinahitajika wakati huu ambapo uhaba wa chakula ni dhahiri.

Kwa sasa kiasi cha dola millioni 95 kinahitajika kwa ajili ya chakula na lishe pamoja na mlo wa dharura kwa ajili shule. Tayari WFP imeandaa mifumo yote muhimu ya ndani ya nchi kabla ya uwezeshaji kifedha wa operesheni na kuzindua manunuzi ya awali ili kukidhi mahitaji ya dharura na ya kipaumbele kwa mwezi Januari na Februari.

WFP inasema hali hiyo pia imesababishwa na kukwama kwa malori mpakani mwa CAR na Cameroon. Inakadiriwa kuwa malori 400 yamekwama ikiwamo 48 ya WFP yenye chakula na misaada mingine ya kiutu. Hifadhi ya manunuzi ya WFP nchini CAR haitoshi.

Katika siku za hivi karibuni shirika hilo la mpango wa chakula duniani limeazima bidhaa na kubadilishana mchele kwa mlo wa mahindi lakini sasa WFP inasema hatua hizi za kukabiliana na ukwasi wa fedha zimeelemewa na shirika litalazimika kutoa pungufu ya mgawo kuanzia January 20 na kusimamisha mgawo nje ya uwanja wa ndegena Bossangoa