Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saa 24 za ulinzi wa amani zahitaji umakini: Private Baruti

Mlinda amani Private Nuru Baruti. (Picha@UNAMID)

Saa 24 za ulinzi wa amani zahitaji umakini: Private Baruti

Mmoja wa walinda amani kwenye ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, Sudan amesema mafunzo aliyopata na ushirikiano kutoka kwa wakuu na askari wenzake ndivyo vinavyomtia moyo kila uchao licha kutekeleza jukumu hilo kwenye mazingira magumu

Private Nuru Baruti ambaye eneo lake la kikazi ni huko Khor Abeche amesema hayo alipozungumza na Idhaa hii wakati  huu wa maadhimisho ya siku ya walinda amani duniani.

 (Sauti ya Baruti)

Askari huyo akazungumzia tukio la hivi karibuni kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani, IDPs ambalo anajivunia..

(Sauti ya Baruti)