Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakumbuka walinda amani waliopoteza maisha wakiwa kazini:Ban

Shada la maua lililowekwa na Katibu Mkuu wa UM kwenye eneo maalum la kumbukumbu ya walinda amani katika makao makuu ya UM. (Picha: M/Devra Berkowitz)

UM wakumbuka walinda amani waliopoteza maisha wakiwa kazini:Ban

Ikiwa leo ni siku ya walinda amani duniani hapa Umoja wa Mataifa kumefanyika matukio maalum kuenzi siku hiyo ikiwemo ile ya Katibu Mkuu Ban Ki-Moon kuweka shada la maua kwenye eneo maalum la kumbukumbu, halikadhalika kutoa medali maalum ya Dag Hammarskjöld kwa walinda amani 106 walifariki dunia wakiwa kazini. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Shughuli ilianza kwa dakika moja ya ukimya kabla ya kuweka shada la maua kukumbuka walinda amani 106 waliopoteza maisha wakihudumu mwaka 2013 pekee.  

Baadhi waliuawa kwenye mashambulizi ilhali wengine walikumbwa na magonjwa na hata kusombwa na mafuriko. Ban amesema vitisho dhidi ya ulinzi wa amani bado kubwa huko Syria, Jamhuri ya Afrika ya Kati, DRC, Mali na kwingineko na Umoja wa Mataifa unajitahidi kupunguza athari.

“Umoja wa Mataifa unafanya kila iwezalo kulinda watendaji wake walioko kwenye operesheni. Licha ya jitihada hizo hatuwezi kupunguza hatari zote kabisa. Ndio maana leo tunasifu ujasiri, kujitoa kwa dhati na weledi wa walinda amani 120,000 walioko sehemu hatari zaidi duniani. Ninawapatia shukrani zangu za dhati kabisa.”

Hatimaye ikafuata utoaji nishani, majina yao na nchi 38 wanazotoka yalisomwa…

Na katika Mkuu akasema kinachomsikitisha kila mara…

Moja ya jukumu gumu ninalofanya mara kwa mara ni kuandika barua kwa serikali kupitia balozi zao kuwajulisha kuwa Fulani amefariki kwenye ulinzi wa amani, tafadhali tuma salamu zangu za rambirambi kwa familia. Baadhi yenu mnapokea mara kwa mara, Natarajia punde sitoandika tena barua hizi. Hivyo tuongeze juhudi ya kusaka amani na utulivu kwani uhai wa kila mtu ni wa kipekee kama mwingine yeyote.”