Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia za kisasa kwenye ulinzi wa amani hazikwepeki:DPKO

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa Herve Ladsous akiangalia moja ya ndege zinazoruka angani bila rubani huko Goma, DRC. (Picha:MONUSCO/Sylvain Liechti)

Teknolojia za kisasa kwenye ulinzi wa amani hazikwepeki:DPKO

Naibu Mkuu wa masuala ya operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Edmond Mulet amesema teknolojia mpya za ulinzi wa amani hazikwepeki wakati huu ambapo mwelekeo na aina ya mizozo hata barani Afrika inabadilika.

Mulet ametaja teknolojia hizo kuwa ni pamoja na ndege zinazorushwa bila rubani, vifaa vya kisasa vya kupata picha za satelite na vile vya mawasiliano ..

(Sauti ya Mulet)

“Dunia inabadilika, vitisho vinabadilika, kiwango cha mizozo kinabadilika kweney sehemu bali mbali duniani, hivyo tunapaswa kwenda na mazingira na kubadilika, kufahamu na kujifunza ni jinsi gani tunaweza kuzishughulikia.”

Amesema ndege zisizo na rubani zimekuwa na manufaa makubwa huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC na watahitaji mfumo kama huo Mali na penginepo Jamhuri ya Afrika ya Kati. Amesema nchi wanachama zimeonyesha mwitikio mkubwa kwenye kutekeleza hilo.